Jumanne, 29 Novemba 2016

UMUHIMU WA UTOAJI SADAKA KIROHO NA KIMWILI PIA

    Kutokutoa zaka na dhabihu ni kumwibia Mungu. Mtu aliye mkristo asipotoa zaka na dhabihu anaitwa mwizi. Kuna wakristo ambao ni wezi lakini wao hawajui yakuwa ni wezi. Wamemwibia Mungu zaka na dhabihu. Mungu anasema hivi:              “Je! mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia ZAKA na DHABIHU” (Malaki 3:8)           Kati ya amri tulizopewa na Mungu ni kwamba tusiibe. Kuiba ni dhambi. Na dhambi ina adhabu yake. Popote palipo na dhambi, laana hutokeza. Kwa wale wanaomwibia Mungu kwa kutokutoa zaka na dhabihu, wamefunikwa na laana. Ndiyo maana Mungu alisema hivi:                 “….. Mmeniibia Zaka na Dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana;   maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote  (Malaki 3:8b, 9).           Laana maana yake ni kutokufanikiwa, kutofaulu, kutokustawi, kukosa furaha, kukosa amani, na kukosa mwelekeo sahihi. Ni wazi kuwa wakristo wengi hawana furaha, hawana amani na hawafanikiwi katika maisha yao ya kila siku, kwa sababu hawamtolei Mungu zaka na dhabihu.             Unapokosa kumtolea Mungu ili ujenzi wa nyumba yake – kanisa uendelee, Hagai 1:6 anatuambia Mungu anasema hivi;             “Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka”. Zaka ni kitu gani?             Zaka ni fungu la kumi la pato lako. Hebu isome na kuitafakari mistari ifuatayo;            “Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana, ni takatifu kwa Bwana ….Tena zaka yote ya ng’ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; SEHEMU YA KUMI watakuwa ni watakatifu kwa Bwana” (Mambo ya Walawi 27:30 –32).             “…Toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako; na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako,  akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo”(Kumbukumbu la Torati 14:28-29).           Zaka ni fungu la kumi la pato toka mshahara wako ofisini, shambani au kwenye mifugo. Tena zaka hii ni ya Bwana na ni Takatifu.                   Mtu asipoitoa zaka hii anamwibia Mungu. Zaka si yako hustahili kukaa nayo wala kuitumia nje ya utaratibu wa Mungu.                   Lakini Malaki 3:10a anasema; “Leteni zaka KAMILI ….” Maana yake nini maneno haya? Maana yake ni hii; ikiwa kwa mfano mshahara wako kwa mwezi ni shilingi 2,000/= ( kabla ya makato) – fungu la kumi au zaka unayotakiwa kutoa ni shilingi 200/= ambayo ndiyo zaka kamili ya mshahara wako. Ukileta pungufu yake hiyo si zaka kamili.                        Tena kwa mfano umevuna magunia 10 ya mahindi toka shambani mwako – zaka kamili unayotakiwa kutoa ni gunia moja bila kupungua. Kumbuka mzaliwa wa kwanza wa mifugo yako ni wa Bwana.                       Unaweza ukasema habari za kutoa zaka ni za agano la kale na siyo za agano jipya.           Waebrania 7:5-10 inatuambia wazi ya kuwa Ibrahimu alitoa fungu la kumi. Kama Ibrahimu alitoa sehemu ya kumi, Je! si zaidi sana kwetu sisi tulio uzao wake kwa imani ndani yake Kristo? Maana imeandikwa hivi;             “Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu na warithi sawasawa na ahadi” (Wagalitia 3:29). Soma pia Wagalitia 3:13,14). Dhabihu ni kitu gani?           Dhabihu ni matoleo yanayotolewa baada ya kutoa sehemu ya kumi ya pato lako. Kwa mfano, kama mshahara wako kwa mwezi ni shilingi 2,000/=, basi sehemu ya kumi (zaka) ni shilingi 200/=. Kiasi cho chote utakachotoa ju ya shilingi 200/= ndiyo matoleo yako. Kwa mfano ukitoa shilingi 210/= toka kwenye mshahara wako wa shilingi 2000/=, Basi, shilingi 200/= ni zaka; na shilingi 10/= ni dhabihu au matoleo au sadaka ya kawaida.           Kiasi utakachotoa katika dhabihu/matoleo, ndicho kitakachokuwa kipimo kitakachoweka kiwango chako cha kupokea. Imeandikwa hivi:             “Lakini nasema neno hili, APANDAYE HABA ATAVUNA HABA; APANDAYE KWA UKARIMU ATAVUNA KWA UKARIMU. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, MKIWA NA RIZIKI ZA  KILA NAMNASIKUZOTE,mpatekuzidisanakatikakilatendojema;kamailivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, haki yake yakaa milele. Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye ATAYAONGEZA MAZAO YA HAKI YENU, MKITAJIRISHWA KATIKA VITU VYOTE MPATE KUWA NA UKARIMU WOTE; umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. Maana utumishi wa huduma hii HAUWATIMIZII WATAKATIFU RIZIKI WALIZOPUNGUKIWA TU, Bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu; kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, WANAMTUKUZA MUNGU kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote” (2Wakorintho 9:6-13)           Soma tena mistari hiyo hapo juu, lakini sasa tafakari zaidi maneno niliyoyaandika kwa herufi kubwa. Utaona kuwa usipokuwa mwaminifu katika utoaji, wewe mwenyewe unakosa kufanikiwa, na pia unamkosesha Mungu shukrani na utukufu ambao angepata kwa utoaji wako. Zaka na dhabihu zitolewe wapi?           Hili jambo linahitaji uongozi wa Roho Mtakatifu, ili upate ufahamu Mungu anataka upeleke wapi zaka na matoleo uliyo nayo.            Hili ni muhimu kwa kuwa Biblia inazungumza juu ya kupeleka kanisani (Malaki 3:10-11), kwa watakatifu (2Wakorintho 9:12), kwa maskini (2Wakorintho 9:8-9), kwa watumishi wa Mungu (1Wafalme 17:10-24; 1Wakorintho 9:7-14); kwa wajane, - na kadhalika.               Muombe Mungu akuongoze mahali pa kupeleka. Amani ya Kristo na iamue moyoni mwako. Baraka Tele!           Kuna baraka tele za mafanikio kwa mkristo aliye mwaminifu katika kumtolea Mungu zaka na matoleo.           Katika Malaki 3:10 imeandikwa hivi; “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo (YA UTOAJI) asema Bwana wa Majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na KUWAMWAGIENI BARAKA, HATA ISIWEPO NAFASI YA KUTOSHA AU LA”.            Je! umewahi kukutana na mkristo ambaye anashuhudia kuwa Mungu amempa baraka nyingi hata HANA MAHALI PA KUZIWEKA? Ni wazi kuwa ahadi hii haijatimia kwa kuwa hatujawa watendaji na Neno kikamilifu katika utoaji.               Soma mistari hii hapa chini uone baraka zingine zinazotokana na utoaji; “Azaria Kuhani Mkuu, wa nyumba ya Sadoki, akamjibu, akasema, Tangu watu walipoanza kuleta matoleo nyumbani kwa Bwana, tumekula na KUSHIBA NA KUSAZA TELE; kwa kuwa Bwana amewabariki watu wake; na kilichosalia ndiyo akiba hii kubwa. Ndiko Hezekia akaamuru kutengeneza vyumba nyumbani mwa Bwana; wakavitengeneza. Wakayaingiza MATOLEO na ZAKA na vitu vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu ….” (2Mambo ya Nyakati 31:10-12).           Kwa nini wakristo wengine wanapungukiwa vyakula, wakati tuna nafasi ya kumruhusu Mungu kutubariki kwa vyakula tele? Mpe Mungu nafasi ya kukubariki kwa kumtolea zaka na matoleo! Anza Sasa!              Nakushauri ya kuwa kama ulikuwa hutoi sehemu ya kumi au zaka pamoja na  matoleo ya kutosha – anza sasa.              Jambo la kwanza, kumbuka kutubu kwa Mungu katika Jina la Yesu Kristo kwa kuwa ulimwibia zaka na dhabihu kwa kutokumtolea.           Halafu mwombe Mungu akuwezeshe kusimama katika uaminifu wa kumtolea zaka na dhabihu ili apate nafasi ya kukubariki zaidi kama tulivyoona, na kama alivyoahidi MUNGU AKUBARIKI. 

        GLORY BE WITH YOU OUR LORD JESUS CHRIST
  
By.  Mwalimu 
                   Israel Kessy

Jumanne, 27 Septemba 2016

               JE?WOKOVU NI NINI?NAO WATUSAIDIA NINI?
      
Bwana Yesu Kristo asifiwe ndugu katika Kristo Yesu.
    Wapendwa    Imempendeza Mungu leo tuangalie kwa kifupi nini maana ya wokovu.Mungu atusaidie na ayafungue masikio yetu ya ndani ili tuelewe na neno hili.Roho ambaye ni mwalimu wa kweli na atusaidie
         Sasa tutaenda kwa mtiririko huu
1.WOKOVU NI NINI?

     kwa lugha nyepesi kabisa na ya kawaida,wokovu ni hali ya kutoka katika hatari au hali mbaya au mabaya kuingia ktk mema.hiyo ni lugha nyepesi kabisa ambayo mtu yeyote anaweza kuelewa,

  Wokovu kibiblia ni:HALI YAKUHAMISHWA TOKA UFALME WA GIZA NA KUPELEKWA KATIKA KATIKA UFALME WA MUNGU,KATIKA NURU NA KUWA NURU KWELI KWELI,NI KUACHA DHAMBI KUMKIRI NA KUMKUBALI YESU KRISTO HUKU UKIAMINI KUWA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO. "kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa ni BWANA na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu,utaokoka,kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata Haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu" (warumi 10:9&10)
     Hapo tunaona yakuwa wokovu ni jambo lakiimani,,pasipo imani mtu yeyote hawezi kuokoka na sio tu kuokoka Bali hata kumpendeza Mungu.biblia inasema "wala pasipo imani haifai kumpendeza Mungu" 
    Kwahiyo wokovu ni kuhamishwa(kiroho) kutoka ufalme wa giza(yaani chini ya milki ya ibilisi shetani)na kuletwa katika ufalme wa NURU(yaani wa Mungu katika furaha,Amani na kushinda daima),kufa na kufufuka katika Kristo(na hapo hatuwi tena sisi Bali Kristo ndani yetu nguvu ya msalaba)   ".........................maana kwa kule kufa kwake,aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake,amwishia Mungu,vivyo hivyo nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Munguvkatika Kristo Yesu.

   Baada ya kuona kidogo maana ya wokovu sasa basi na tuelekee kipengele cha pili kuangalia je wokovu tukiupata ukiwa ndani mwetu utatusaidia nini? Karibu tuende pamoja

     2.WOKOVU UNATUSAIDIA NINI?

Wapendwa wengi sana ukiwauliza leo wokovu unawasaidia nini wengine watakuambia unawasaidia kwenda mbinguni tu na wengine watakuambia ni njia yakujipatia kitu fulani has a Mali na vitu vifananavyo na hivyo,
   pamoja na kwamba wokovu hutusaidia mambo mengi sana ila wacha tuone mambo makuu ambayo tunayapata tukiwa na wokovu

               WOKOVU HUTUSAIDIA MAMBO MAKUBWA MAWILI (2 main things)

  • Ni tiketi (ticket) ya kwenda mbinguni (Yohana 14:6,Tito 3:7)
  • Hutusaidia kuishi maisha ya furaha na maisha ambayo Mungu ametupangia kuishi katika kusudi lake hapa duniani.(ebrania 4:16)

   1.NI TICKET YA KWENDA MBINGUNI
 Tokea mwanzo Mungu alimuumba mwanadamu ili awe karibu naye,ili azungumze naye wazi,ili amuone waziwazi, lakini kutokana na dhambi aliyoifanya Adam katika bustani ya Eden ilimfanya Mungu awe mbali na wanadamu,dhambi ile iliufanya ulimwengu wote uwe chini ya laana ya dhambi ambayo hadi leo inausumbua ulimwengu, ndugu zangu napenda mjue hili,hata kama mtu anatenda mema kwa namna gani hawezi kusema ataenda mbinguni,hii ni kwa sababu mbinguni hatuendi kwa haki ipatikanayo kwa matendo yakisheria,la! Bali kwa imani kisha haki tuipatayo kwa NEEMA  ya Kristo Yesu.hakuna namna ambavyo unaweza kuingia mbinguni kama unategemea kwa matendo yako ndugu ila ni kwa kukiraribia kitu cha neema tu nyakati zote,wala sisi tuliookoka tusijisifu kwa kuwa tumeokoka,Bali tuzidi kukisogelea hicho kiti cha Rehema na neema "KWA MAANA MMEOKOLEWA KWA NEEMA,KWA NJIA YA IMANI AMBAYO HIYO HAIKUTOKANA NA NAFSI ZENU ILA NI KIPAWA CHA MUNGU.WALA SI KWA MATENDO MTU YEYOTE ASIJE AKAJISIFU" (waefeso 2:8&9) HALLELUYA..ndugu hakuna fahari kama hii yakukombolewa,maanake sio tu kwamba tunashinda katika ulimwengu huu ila pia tunazo ahadi za kuingia katika ufalme wa Mungu katika kutawala pamoja na Kristo baada ya dhiki za hapa.
       Wakati mwingine tutaendelea na kipengele cha pili,  Ila kwa sasa chukua hatua hii muhimu kwa kufuatilia kwa makini maneno haya muhimu hapa chini.

  Ndugu zangu wokovu si kitu cha kudharau wala kusema nitasubiria kesho au wakati mwingine maana hatuijui sekunde moja ya maisha yetu yajayo itakuwaje,Fikiria leo upo kesho haupo,leo unaishi kesho mwili umeacha roho,utaelekea wapi?Biblia inasema zipo hatima mbili, jehanamu na Paradiso ya milele,hakuna sehemu nyingine,je? wewe utapenda kwenda Jehanamu? naamini jibu litakuwa hapana kabisa,Kama usingependa kwenda jehanamu INA maana ungependa kwenda MBINGUNI,hivyo ni vyema kutengeneza mambo yako sasa,
    KAMA UPO TAYARI KUOKOKA FUATISHA MANENO HAYA NA CHUKULIA KWA IMANI KUWA NIWEWE UNAYASEMA TOKA MOYONI NA YESU ACHUNGUZAYE MIOYO ATAKUOKOA

   SEMA:ee Mungu baba, ninakuja kwako,mimi mwenyewe dhambi,ninaungama mbele zako dhambi zangu zote nilizozifanya,nakuja mbele za kiti chako cha neema nakusihi unisamehe na kunipa rehema.naomba ufute jina langu katika kitabu cha hukumu na kuandika jina langu katika kitabu cha uzima, asante Yesu kwa kuniokoa na kunifia pale msalabani,nipe kukujua wewe,nitembee ndani yako sikuzote,dhambi isinishinde,shetani asinishe,nidumu ndani yako siku zote za maisha yangu. 

      Ameen.
Umefanya uamuzi wa busara sana hii leo.Mungu wa mbinguni akutunze siku zote za maisha yako.2Timothy 4:18 biblia inasema ivi "Bwana ataniokoa na kila neno baya na kunihifadhi hata nifike ufalme wa MBINGUNI. Mungu akuhifadhi ndugu hata ufike salama

  Neema na iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo katika hali ya kutokuharibika
   By
              Mwalimu Israel Kessy

      Phone number     0783_872656

      e_mail address    israelkessy@gmail.com

      Facebook              Israel Kessy (mwalimu Kessy)

Ijumaa, 19 Agosti 2016

HUKUMU YA SIKU ZA MWISHO PAMOJA NA UHALALI WA UENDAPO

Menu

O————————————– BAADA YA KUOKOKA,TAFUTA UTAKATIFU

A————————————————————————————– — YOHANA 17:17 & WAEBRANIA 12:14

KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU

.

  SOMO:   KITI  CHA    KIKUBWA  CHEUPE   CHA  HUKUMU 

                                                                       (  UFUNUO 20:11-15  )

Baada tu ya vita vya Gogu na Magogu vitakavyofanyika mwishoni mwa miaka elfu moja ya Utawala wa Yesu Kristo duniani, kutafuata ufufuo wa pili unaoitwa pia ufufuo wa Hukumu ( YOHANA 5:28-29  ) . Huu ni ufufuo wa wale waliotenda mabaya, yaani wote wenye dhambi waliokufa pasipo utakatifu, tangu nyakati za mwanzo kabisa za vizazi vya Adamu hadi wale wote watakaoliwa na moto kwenye Vita vya Gogu na Magogu (UFUNUO 20:7-9 ) . Hawa wote baada ya kufa kwao wamekuwa katika kipindi chote hicho kwenye mateso makali Jehanum ya moto . Hawa, watafufuliwa na kuirudia miili yao ya asili na kusimama mbele ya Kiti cha Enzi Kikubwa Cheupe cha Hukumu . Ili tuelewe yale yatakayofanyika hapa, tutaligawa somo letu katika vipengele saba.

( 1 )   HAKIMU ATAKAYEKALIA KITI CHA ENZI KIKUBWA

CHEUPE CHA HUKUMU

( 2 )   MAKUSUDI YA HUKUMU YA KITI CHA ENZI KIKUBWA

CHEUPE

( 3 )  WINGI WA WATU WATAKAOHUKUMIWA

( 4 )  WADOGO PIA KUHUKUMIWA

( 5 )   KIPIMO KITAKACHOTUMIWA KATIKA HUKUMU

( 6 )   KUFUNULUWA KWA SIRI ZOTE MBELE YA MASHAHIDI

WA MUNGU

( 7 )   HUKUMU YA MWISHO

( 1 )  HAKIMU ATAKAYEKALIA KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA

         HUKUMU

Hakimu atakayekikalia kiti hiki ni Yesu Kristo . Yeyote leo anayemkana Yesu Kristo kuwa siyo mwana wa Mungu , atafahamu hapa kwamba hukumu yote iko chini yake ( YOHANA 5:22 ; MATENDO 10:38-41; 17:31; WARUMI 2:16; 2TIMOTHEO 4:1 ). Ni heri kufahamu mapema hivi leo kwamba Yesu ndiye hakimu na kuomba msamaha kwake, yeye yuko tayari kulehemu na kusamehe kabisa ( ISAYA 55:6-7 ). Yesu atakapokikalia kiti cha enzi kikubwa cheupe atakuwa mwenye hasira, huruma itakuwa mbali naye kabisa EZEKIELI 7:4; 8:18; WARUMI 2:4-5 ).

( 2 ). MAKUSUDI YA HUKUMU YA KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE.

Hukumu hii, haitakuwa na makusudi ya kuwaweka huru wenye dhambi fulani fulani. Ilivyo ni kwamba yeyote yule asiyemwamini Yesu Kristo hadi kufa kwake, ghadhabu ya Mungu inamkalia ( YOHANA 3:36 ). Mtu yeyote mwenye dhambi anapokufa, huenda motoni moja kwa moja. Mtu huyu huenda motoni bila kuelezwa ni kwa nini anapelekwa kwenye mateso hayo.   Makusudi ya hukumu hii itakuwa ni kumfahamisha kila mmoja aliye katika mateso ya Jehanamu uhalali way eye kupewa adhabu hiyo ya milele. Itadhihirishwa kwa kila mmoja mmoja kwamba adhabu ya moto wa milele ni malipo halisi aliyopata kadri ya matendo yake ( WARUMI 2:6 ). Yesu hapa atasimama kama mhukumu wa haki ( MATENDO 17:31 ).

( 3 ). WINGI WA WATU WATAKAOHUKUMIWA

Watu wanaokwenda Jehanum ni wengi sana kuliko wengi wanavyofikilia ( MATHAYO  7:13-14 ). Mbinguni kuna vitabu vya aina mbili, kitabu cha uzima ambamo huandikwa majina ya wale waliookoka ambao hudumu kutenda mapenzi ya Mungu ( LUKA 10:20; WAFILIPI 4:3 ). Wale waliookoka wasiodumu kutenda mapenzi ya Mungu, hufutwa majina yao na kuondolewa katika kitabu mbali na wokovu, majina yao yamo katika vitabu vya kumbukumbu, vitabu vya hukumu. Kwa kuwa watu hawa ni wengi sana, majina yao yako katika VITABU VINGI, lakini wale wa mbinguni wako katika KITABU KIMOJA CHA UZIMA ( UFUNUO 20:12 ). Hatupaswi kudanganyika kutokana na watu wengi wanaosema wameokoka huku maisha yao hayako nuruni na kufikiria kwamba wote hawa wataingia mbinguni. Gharika iliwaangamiza watu wote duniani na  kubakiaWANANE TU walioingia safinani. Viwango vya Mungu vya utakatifu havibadiliki ( MATHAYO 5:48; 1PETRO 1:15-17; WAEBRANIA 12:14 ).

( 4 ). WADOGO PIA KUHUKUMIWA.

Wakubwa kwa wadogo, watakuwepo kwenye hukumu hii ( UFUNUO 20:12 ). Ni muhimu kuwashuhudia injili watoto wetu wadogo walio na akili ya kujua mema na mabaya, na kuwapa nafasi ya kutubu, na kuokolewa; au sivyo, tutahuzunika kuwaona wakiwa kwenye hukumu hii, wakiwa wametoka kwenye mateso ya moto. Mtoto mdogo mwenye uwezo wa kufahamu hesabu ya59 + 68 ana upeo mkubwa wa kufahamu mema na mabaya. Katika injili yetu kwa watoto wa jinsi hii, tunatakiwa kutaja dhambi wanazoweza kuzielewa. Wizi wa kalamu, uongo, kutokuwatii na kuwaheshimu wazazi  n.k, baada ya mtoto kumwamini Yesu, huongozwa sara ya Toba. Baada ya hapo, fahamu kuwa ameokoka na endelea kumfundisha bila kubabaishwa na mambo ya kitoto anayofanya siku kwa siku. Ni muhimu kukumbuka kwamba ni watoto wadogo kabisa wasioifahamu sheria ambao ufalme wa mbinguni ni wao. Wengi wao huwa bado wana umri wa kukumbatiwa ( MARKO 10:13-16; WARUMI 4:15; 5:13 ).

( 5 ). KIPIMO KITAKACHOTUMIWA KATIKA HUKUMU.

Watu wengi wanafanya makosa makubwa pale wanapofikiria kwamba, watakwenda mbinguni kutokana na kufanya mambo yaliyo sana na mafundisho ya madhehebu yao au mchungajiwao.Hiki siyo kipimo kitakachotumiwa na Yesu katika hukumu. Wengi wanaojifariji kwa kutenda yaliyo halali kwa wachungaji wao au madhehebu yao, ingawa yako tofauti na maagizo ya Neno la Mungu; watakwenda katika mateso ya moto wa milele. Kipimo atakachotumia Yesu katika hukumu ni NENO LA MUNGU au INJILI ( WARUMI 2:16 ). Ni muhimu kuyalinganisha yale tunayoyafanya  na Neno la Mungu  na siyo mafundisho  ya madhehebu yetu  au Wachungaji na Maaskofu  wanaotuambia kufanya hili na lile  siyo lazima ( ZABURI 119:6, 9 ). Siyo hilo tu, kipimo cha Yesu katika hukumu kitakuwa  Neno la Mungu. Wale ambao hawakuwa  na Biblia kijijini kwao, wale ambao walikuwa mahali pasipokuwa na mafundisho, wale ambao walikatazwa na wazazi wao kuwa Wakristo, wote hawa watapotea  pasipo kuifahamu sheria.. Kukosa kufahamu yaliyo halali siyo udhuru utakaokubalika. Wale wanaoyafahamu mafundisho lakini hawayatendi waon pia wataangamia pamoja na kuyajua hayo ( MAMBO YA  WALAWI 5:17; WARUMI 2:11-14 ). Mungu anamtarajia kila mwanadamu kuyatafuta mafundisho ya kweli hata iwe mbali kiasi gani kama alivyo tayari kufuata elimu Ulaya au biashara nchi za nje ( MATHAYO 12:42 ).

( 6 ). KUFUNULIWA KWA SIRI ZOTE MBELE YA MASHAHIDI WA MUNGU.

Mmojammoja atasimama mbele ya kiti hicho cha Enzi kikubwa cheupe. Mahali hapo itakuwa ni aibu na kudharauliwa ( DANIELI 12:2 ). Kila mmoja ataonyeshwa matendo yake, maneno yake, mawazo yake na nia yake kwa mfano wa VIDEOiliyotuzwa kumbukumbu zake. Siri zote za wanadamu zitakuwa wazi hapo ( AYUBU 20:27; METHELI 26:26; MHUBIRI 22:14; LUKA 12:2; 1WAKORINTHO 4:5; WARUMI 2:16 ). Mahali hapo utawaona wahubiri wazinzi. Kila kitu kitaonyeshwa WAZIWAZI. Hatua zote za mtu kumshawishi mwanamke wa mtu hadi kuingia naye nyumba ya kulala wageni na kufanya uchafu wote, vyote vitaonyeshwa hapo mbele ya wote. Maneno yote ya mtu anayoyatamka, yatawekwa wazi hapo, na kwa kila neno mtu atahukumiwa ( MATHAYO 12:36-37 ). Mtu aliyekuwa anahudhuria mikutano ya injili bila kukata shauri kuokolewa, atajiona picha yake akiwa katika mikutano hiyo na wakati akirudi nyumbani atajiona anasema “siwezi kuokoka”. Wala walioshindwa kufanya hili na lile kwa visingizio kuwa ni wanajeshi, ni vijana wadogo n.k watawaona mashahidi wa Mungu walioyafanya waliyoyakataa wakiwa na hali zao. Watakatifu watakuwepo kuona kila mtu na kuwa mashahidi wa Mungu ( WAEBRANIA 12:1; MATHAYO 12:42; MALAKI 3:18; 4:1-2 ).

( 7 ). HUKUMU YA MWISHO.

Watu watajitetea kwa kilio hapo na kisema “mimi nilifanya miujiza kwa jina lako”, “mimi nilitoa pepo kwa jina lako”, mimi nilishuhudia na kufuatilia n.k, na Yesu atasema sikuwajua ninyi; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu ( MATHAYO 7:22-23 ). Kila mtu atatolewa hapo na kukamatwa kwa nguvu kisha atatupwa kwenye ZIWA LA MOTO.Ziwa la moto ni tofauti na kuzimu au Jehanum. Ziwa la moto kwa sasa halina mtu ndani yake. Wa kwanza kutupwa humo watakuwa Mnyama au mpinga Kristo na nabiii wa uongo ( UFUNUO 19:20 ). Kisha atafuata Shetani ( UFUNUO 20:10 ). Mateso ya ziwa la moto ni mazito zaidi kuliko Jehanum. Mauti au kifo ni Jehenum ya sasa, vyote pia vitatupwa katika ziwa la moto pamoja na wenye dhambi wote ( UFUNUO 20:14-15, 21:8 ). Hapo itakuwa “kwaheri ya kutokuonana tena” kwa wenye dhambi na watakatifu.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Mpendwa msomaji, baada ya kusikia yote haya kutoka kwa nabii aliyetumwa kukuletea ujumbe huu, usifanye moyo wako kuwa mgumu.  Hii ni nafasi ya kipekee ya kuokoka.  Je, unajuaje kama utaamka kitandani baada ya kulala usiku wa leo?  Wakati uliokubalika wa wokovu ni sasa (2 WAKORINTHO 6:2).  Labda utaniuliza, ili uokoke, ufanyeje?  Jibu ni rahisi, kwa imani ukitubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, na kumwambia Yesu Kristo akusamehe, utasamehewa sasa hivi, na msamaha wa dhambi, huambatana na wokovu (LUKA 1:77).  Je, uko tayari kuokoka sasa hivi?  Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii kwa dhati toka moyoni, Mungu baba asante kwa kuniletea ujumbe huu.Natubu dhambi zangu zote, kwa kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo nakuomba unisamehe dhambi zangu na kunipa uwezo wa kushinda dhambi na kuniokoa kutoka katika mateso ya moto wa milele. Asante, kwa kuniokoa katika Jina la Yesu.  Amen.  Tayari sasa umeokoka, na kwa hakika unakwenda mbinguni sasa, hata ukifa leo.  Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

Masomo ya matukio ya mwisho wa Dunia. Unaweza kuingia kwenye link ya kila somo.
1. KUNYAKULIWA KWA KANISA
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/01/02/kunyakuliwa-kwa-kanisa/
2. DHIKI KUBWA
https://davidcarol719.wordpress.com/dhiki-kubwa/
3. TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/taji-kwa-watakatifu-na-harusi ya-mwanakondoo/
4. KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA VYA HAR-MAGEDONI
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/kuja-kwa-yesu-kristo-mara-ya-pili-duniani-na-vita-ya-har-magedoni/
5. MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI NA VITA VYA GOGU NA MAGOGU
https://davidcarol719.wordpress.com/miaka-1000-ya-utawala-wa-yesu-kristo-duniani-na-vita-vya-gogu-na-magogu/
6. UFUFU WA WAFU
https://davidcarol719.wordpress.com/187-2/
7. JEHANUM YA MOTO
https://davidcarol719.wordpress.com/jehanum-ya-moto/
8. KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU
https://davidcarol719.wordpress.com/?s=KITI+CHA+ENZI+KIKUBWA+CHEUPE+CHA+HUKUMU
9. MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
https://davidcarol719.wordpress.com/mbingu-mpya-na-nchi-mpya/

               . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook, Twitter n.k  kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

UBARIKIWE SANA KWA KAZI YAKO NJEMA

Share this:

TwitterFacebook185

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Comment 

Name*

Email*

Website

 Notify me of new comments via email.

Recent Posts

THE REVIVALIST TO THE NATIONS, BISHOP ZACHARY KAKOBEUSHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU NA YERUSALEMU MPYA WA NYISAKI CHAULAAMANI YA KRISTO IAMUE MIOYONI MWENUSAUTI YA MUNGUKUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA YA HAR-MAGEDONI

Archives

February 2014December 2013May 2013February 2013January 2013

Categories

Uncategorized

Meta

RegisterLog inEntries RSSComments RSSWordPress.com

View Full Site

Blog at WordPress.com.

         By  
                Mwl    Israel Kessy
                              From
       Mch Kakobe

Alhamisi, 18 Agosti 2016

Kweli

Menu

O————————————– BAADA YA KUOKOKA,TAFUTA UTAKATIFU

A————————————————————————————– — YOHANA 17:17 & WAEBRANIA 12:14

KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU

  Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook :www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   :www.youtube.com/user/bishopkakobe

  SOMO:   KITI  CHA  ENZI  KIKUBWA  CHEUPE   CHA  HUKUMU 

                                                                       (  UFUNUO 20:11-15  )

Baada tu ya vita vya Gogu na Magogu vitakavyofanyika mwishoni mwa miaka elfu moja ya Utawala wa Yesu Kristo duniani, kutafuata ufufuo wa pili unaoitwa pia ufufuo wa Hukumu ( YOHANA 5:28-29  ) . Huu ni ufufuo wa wale waliotenda mabaya, yaani wote wenye dhambi waliokufa pasipo utakatifu, tangu nyakati za mwanzo kabisa za vizazi vya Adamu hadi wale wote watakaoliwa na moto kwenye Vita vya Gogu na Magogu (UFUNUO 20:7-9 ) . Hawa wote baada ya kufa kwao wamekuwa katika kipindi chote hicho kwenye mateso makali Jehanum ya moto . Hawa, watafufuliwa na kuirudia miili yao ya asili na kusimama mbele ya Kiti cha Enzi Kikubwa Cheupe cha Hukumu . Ili tuelewe yale yatakayofanyika hapa, tutaligawa somo letu katika vipengele saba.

( 1 )   HAKIMU ATAKAYEKALIA KITI CHA ENZI KIKUBWA

CHEUPE CHA HUKUMU

( 2 )   MAKUSUDI YA HUKUMU YA KITI CHA ENZI KIKUBWA

CHEUPE

( 3 )  WINGI WA WATU WATAKAOHUKUMIWA

( 4 )  WADOGO PIA KUHUKUMIWA

( 5 )   KIPIMO KITAKACHOTUMIWA KATIKA HUKUMU

( 6 )   KUFUNULUWA KWA SIRI ZOTE MBELE YA MASHAHIDI

WA MUNGU

( 7 )   HUKUMU YA MWISHO

( 1 )  HAKIMU ATAKAYEKALIA KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA

         HUKUMU

Hakimu atakayekikalia kiti hiki ni Yesu Kristo . Yeyote leo anayemkana Yesu Kristo kuwa siyo mwana wa Mungu , atafahamu hapa kwamba hukumu yote iko chini yake ( YOHANA 5:22 ; MATENDO 10:38-41; 17:31; WARUMI 2:16; 2TIMOTHEO 4:1 ). Ni heri kufahamu mapema hivi leo kwamba Yesu ndiye hakimu na kuomba msamaha kwake, yeye yuko tayari kulehemu na kusamehe kabisa ( ISAYA 55:6-7 ). Yesu atakapokikalia kiti cha enzi kikubwa cheupe atakuwa mwenye hasira, huruma itakuwa mbali naye kabisa (  EZEKIELI 7:4; 8:18; WARUMI 2:4-5 ).

( 2 ). MAKUSUDI YA HUKUMU YA KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE.

Hukumu hii, haitakuwa na makusudi ya kuwaweka huru wenye dhambi fulani fulani. Ilivyo ni kwamba yeyote yule asiyemwamini Yesu Kristo hadi kufa kwake, ghadhabu ya Mungu inamkalia ( YOHANA 3:36 ). Mtu yeyote mwenye dhambi anapokufa, huenda motoni moja kwa moja. Mtu huyu huenda motoni bila kuelezwa ni kwa nini anapelekwa kwenye mateso hayo.   Makusudi ya hukumu hii itakuwa ni kumfahamisha kila mmoja aliye katika mateso ya Jehanamu uhalali way eye kupewa adhabu hiyo ya milele. Itadhihirishwa kwa kila mmoja mmoja kwamba adhabu ya moto wa milele ni malipo halisi aliyopata kadri ya matendo yake ( WARUMI 2:6 ). Yesu hapa atasimama kama mhukumu wa haki ( MATENDO 17:31 ).

( 3 ). WINGI WA WATU WATAKAOHUKUMIWA

Watu wanaokwenda Jehanum ni wengi sana kuliko wengi wanavyofikilia ( MATHAYO  7:13-14 ). Mbinguni kuna vitabu vya aina mbili, kitabu cha uzima ambamo huandikwa majina ya wale waliookoka ambao hudumu kutenda mapenzi ya Mungu ( LUKA 10:20; WAFILIPI 4:3 ). Wale waliookoka wasiodumu kutenda mapenzi ya Mungu, hufutwa majina yao na kuondolewa katika kitabu mbali na wokovu, majina yao yamo katika vitabu vya kumbukumbu, vitabu vya hukumu. Kwa kuwa watu hawa ni wengi sana, majina yao yako katika VITABU VINGI, lakini wale wa mbinguni wako katika KITABU KIMOJA CHA UZIMA ( UFUNUO 20:12 ). Hatupaswi kudanganyika kutokana na watu wengi wanaosema wameokoka huku maisha yao hayako nuruni na kufikiria kwamba wote hawa wataingia mbinguni. Gharika iliwaangamiza watu wote duniani na  kubakiaWANANE TU walioingia safinani. Viwango vya Mungu vya utakatifu havibadiliki ( MATHAYO 5:48; 1PETRO 1:15-17; WAEBRANIA 12:14 ).

( 4 ). WADOGO PIA KUHUKUMIWA.

Wakubwa kwa wadogo, watakuwepo kwenye hukumu hii ( UFUNUO 20:12 ). Ni muhimu kuwashuhudia injili watoto wetu wadogo walio na akili ya kujua mema na mabaya, na kuwapa nafasi ya kutubu, na kuokolewa; au sivyo, tutahuzunika kuwaona wakiwa kwenye hukumu hii, wakiwa wametoka kwenye mateso ya moto. Mtoto mdogo mwenye uwezo wa kufahamu hesabu ya59 + 68 ana upeo mkubwa wa kufahamu mema na mabaya. Katika injili yetu kwa watoto wa jinsi hii, tunatakiwa kutaja dhambi wanazoweza kuzielewa. Wizi wa kalamu, uongo, kutokuwatii na kuwaheshimu wazazi  n.k, baada ya mtoto kumwamini Yesu, huongozwa sara ya Toba. Baada ya hapo, fahamu kuwa ameokoka na endelea kumfundisha bila kubabaishwa na mambo ya kitoto anayofanya siku kwa siku. Ni muhimu kukumbuka kwamba ni watoto wadogo kabisa wasioifahamu sheria ambao ufalme wa mbinguni ni wao. Wengi wao huwa bado wana umri wa kukumbatiwa ( MARKO 10:13-16; WARUMI 4:15; 5:13 ).

( 5 ). KIPIMO KITAKACHOTUMIWA KATIKA HUKUMU.

Watu wengi wanafanya makosa makubwa pale wanapofikiria kwamba, watakwenda mbinguni kutokana na kufanya mambo yaliyo sana na mafundisho ya madhehebu yao au mchungajiwao.Hiki siyo kipimo kitakachotumiwa na Yesu katika hukumu. Wengi wanaojifariji kwa kutenda yaliyo halali kwa wachungaji wao au madhehebu yao, ingawa yako tofauti na maagizo ya Neno la Mungu; watakwenda katika mateso ya moto wa milele. Kipimo atakachotumia Yesu katika hukumu ni NENO LA MUNGU au INJILI ( WARUMI 2:16 ). Ni muhimu kuyalinganisha yale tunayoyafanya  na Neno la Mungu  na siyo mafundisho  ya madhehebu yetu  au Wachungaji na Maaskofu  wanaotuambia kufanya hili na lile  siyo lazima ( ZABURI 119:6, 9 ). Siyo hilo tu, kipimo cha Yesu katika hukumu kitakuwa  Neno la Mungu. Wale ambao hawakuwa  na Biblia kijijini kwao, wale ambao walikuwa mahali pasipokuwa na mafundisho, wale ambao walikatazwa na wazazi wao kuwa Wakristo, wote hawa watapotea  pasipo kuifahamu sheria.. Kukosa kufahamu yaliyo halali siyo udhuru utakaokubalika. Wale wanaoyafahamu mafundisho lakini hawayatendi waon pia wataangamia pamoja na kuyajua hayo ( MAMBO YA  WALAWI 5:17; WARUMI 2:11-14 ). Mungu anamtarajia kila mwanadamu kuyatafuta mafundisho ya kweli hata iwe mbali kiasi gani kama alivyo tayari kufuata elimu Ulaya au biashara nchi za nje ( MATHAYO 12:42 ).

( 6 ). KUFUNULIWA KWA SIRI ZOTE MBELE YA MASHAHIDI WA MUNGU.

Mmojammoja atasimama mbele ya kiti hicho cha Enzi kikubwa cheupe. Mahali hapo itakuwa ni aibu na kudharauliwa ( DANIELI 12:2 ). Kila mmoja ataonyeshwa matendo yake, maneno yake, mawazo yake na nia yake kwa mfano wa VIDEOiliyotuzwa kumbukumbu zake. Siri zote za wanadamu zitakuwa wazi hapo ( AYUBU 20:27; METHELI 26:26; MHUBIRI 22:14; LUKA 12:2; 1WAKORINTHO 4:5; WARUMI 2:16 ). Mahali hapo utawaona wahubiri wazinzi. Kila kitu kitaonyeshwa WAZIWAZI. Hatua zote za mtu kumshawishi mwanamke wa mtu hadi kuingia naye nyumba ya kulala wageni na kufanya uchafu wote, vyote vitaonyeshwa hapo mbele ya wote. Maneno yote ya mtu anayoyatamka, yatawekwa wazi hapo, na kwa kila neno mtu atahukumiwa ( MATHAYO 12:36-37 ). Mtu aliyekuwa anahudhuria mikutano ya injili bila kukata shauri kuokolewa, atajiona picha yake akiwa katika mikutano hiyo na wakati akirudi nyumbani atajiona anasema “siwezi kuokoka”. Wala walioshindwa kufanya hili na lile kwa visingizio kuwa ni wanajeshi, ni vijana wadogo n.k watawaona mashahidi wa Mungu walioyafanya waliyoyakataa wakiwa na hali zao. Watakatifu watakuwepo kuona kila mtu na kuwa mashahidi wa Mungu ( WAEBRANIA 12:1; MATHAYO 12:42; MALAKI 3:18; 4:1-2 ).

( 7 ). HUKUMU YA MWISHO.

Watu watajitetea kwa kilio hapo na kisema “mimi nilifanya miujiza kwa jina lako”, “mimi nilitoa pepo kwa jina lako”, mimi nilishuhudia na kufuatilia n.k, na Yesu atasema sikuwajua ninyi; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu ( MATHAYO 7:22-23 ). Kila mtu atatolewa hapo na kukamatwa kwa nguvu kisha atatupwa kwenye ZIWA LA MOTO.Ziwa la moto ni tofauti na kuzimu au Jehanum. Ziwa la moto kwa sasa halina mtu ndani yake. Wa kwanza kutupwa humo watakuwa Mnyama au mpinga Kristo na nabiii wa uongo ( UFUNUO 19:20 ). Kisha atafuata Shetani ( UFUNUO 20:10 ). Mateso ya ziwa la moto ni mazito zaidi kuliko Jehanum. Mauti au kifo ni Jehenum ya sasa, vyote pia vitatupwa katika ziwa la moto pamoja na wenye dhambi wote ( UFUNUO 20:14-15, 21:8 ). Hapo itakuwa “kwaheri ya kutokuonana tena” kwa wenye dhambi na watakatifu.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Mpendwa msomaji, baada ya kusikia yote haya kutoka kwa nabii aliyetumwa kukuletea ujumbe huu, usifanye moyo wako kuwa mgumu.  Hii ni nafasi ya kipekee ya kuokoka.  Je, unajuaje kama utaamka kitandani baada ya kulala usiku wa leo?  Wakati uliokubalika wa wokovu ni sasa (2 WAKORINTHO 6:2).  Labda utaniuliza, ili uokoke, ufanyeje?  Jibu ni rahisi, kwa imani ukitubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, na kumwambia Yesu Kristo akusamehe, utasamehewa sasa hivi, na msamaha wa dhambi, huambatana na wokovu (LUKA 1:77).  Je, uko tayari kuokoka sasa hivi?  Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii kwa dhati toka moyoni, Mungu baba asante kwa kuniletea ujumbe huu.Natubu dhambi zangu zote, kwa kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo nakuomba unisamehe dhambi zangu na kunipa uwezo wa kushinda dhambi na kuniokoa kutoka katika mateso ya moto wa milele. Asante, kwa kuniokoa katika Jina la Yesu.  Amen.  Tayari sasa umeokoka, na kwa hakika unakwenda mbinguni sasa, hata ukifa leo.  Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

Masomo ya matukio ya mwisho wa Dunia. Unaweza kuingia kwenye link ya kila somo.
1. KUNYAKULIWA KWA KANISA
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/01/02/kunyakuliwa-kwa-kanisa/
2. DHIKI KUBWA
https://davidcarol719.wordpress.com/dhiki-kubwa/
3. TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/taji-kwa-watakatifu-na-harusi– ya-mwanakondoo/
4. KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA VYA HAR-MAGEDONI
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/kuja-kwa-yesu-kristo-mara-ya-pili-duniani-na-vita-ya-har-magedoni/
5. MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI NA VITA VYA GOGU NA MAGOGU
https://davidcarol719.wordpress.com/miaka-1000-ya-utawala-wa-yesu-kristo-duniani-na-vita-vya-gogu-na-magogu/
6. UFUFU WA WAFU
https://davidcarol719.wordpress.com/187-2/
7. JEHANUM YA MOTO
https://davidcarol719.wordpress.com/jehanum-ya-moto/
8. KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU
https://davidcarol719.wordpress.com/?s=KITI+CHA+ENZI+KIKUBWA+CHEUPE+CHA+HUKUMU
9. MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
https://davidcarol719.wordpress.com/mbingu-mpya-na-nchi-mpya/

               . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook, Twitter n.k  kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

UBARIKIWE SANA KWA KAZI YAKO NJEMA

Share this:

TwitterFacebook184

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Comment 

Name*

Email*

Website

 Notify me of new comments via email.

Recent Posts

THE REVIVALIST TO THE NATIONS, BISHOP ZACHARY KAKOBEUSHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU NA YERUSALEMU MPYA WA NYISAKI CHAULAAMANI YA KRISTO IAMUE MIOYONI MWENUSAUTI YA MUNGUKUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA YA HAR-MAGEDONI

Archives

February 2014December 2013May 2013February 2013January 2013

Categories

Uncategorized

Meta

RegisterLog inEntries RSSComments RSSCreate a free website or blog at WordPress.com.

View Full Site

Proudly powered by WordPress

Jumanne, 5 Aprili 2016

MIZIMU NA NAMNA YAKUISHINDA

- Atom
Luka 12:40 - Nanyi jiwekeni
tayari, kwa kuwa saa msiyodhani
ndipo ajapo Mwana wa Adamu.
Maisha ya ushindi

       By mwl israel kessy

KUFUNGULIWA KUTOKA ROHO
ZA MIZIMU
Mizimu (family spirit) ni mapepo
yaliyotokana na malaika walioasi
pamoja na shetani ambayo watu
waliyafanya kama ndugu kutoka
kizazi hadi kizazi.
Mizimu no roho za shetani
ambazo ni chukizo kwa MUNGU
Kumbukumbu 18:9-12
''Utakapokwisha kuingia katika nchi
akupayo BWANA, MUNGU wako
usijifunze kutenda kwa mfano wa
machukizo ya mataifa yale.
Asionekane kwako mtu ampitishaye
mwanawe au binti yake kati ya
moto, wala asionekane mtu
atazamaye bao, wala mtu
atazamaye nyakati mbaya, wala
mwenye kubashiri, wala msihiri,
wala mtu alogaye kwa kupiga
mafundo, wala mtu apandishaye
pepo, wala mchawi, wala mtu
awaombaye wafu. Kwa maana mtu
atendaye hayo ni chukizo kwa
BWANA; kisha ni kwa sababu ya
hayo BWANA, MUNGU wako,
anawafukuza mbele
yako.'' yanayozungumza hapo
tuliposoma ni kuwahusu
WAGANGA WA KIENYEJI,
WACHAWI, WANAJIMU,WASIHIRI
NA WANAOWAOMBA WAFU,
mambo ambayo yote ni
machukizo kwa MUNGU na wote
hawa wanatumia mizimu
kufanikisha mambo yao na kwa
wale wanaomba maiti(wafu)
hawa wanaomba mizimu hivyo
wanahusika moja kwa moja na
mizimu maana mtu aliyekufa
hawezi kamwe kukusikia na hata
kama anakutokea usiku tambua
tu kwamba ni mizimu ambayo ni
majini yanavaa sura ya ndugu
yako na kuja kwako na kumbuka
kuwa jini anaweza kuiga kila kitu
kuanzia sauti hadi sura na kwa
sababu shetani anataka umkosee
MUNGU wako kwa kumtii yeye,
atakuambia mambo mengi ya
kufanya,
Yupo mama mmoja alikua
anatokewa na mama yake na
kumwambia kwamba '' siku hizi
umenisahau kabisa hata
kaburi langu hufagii hivyo
kesho asubuhi sana
kafagie na unyunyuzie
damu ya kuku juu ya
kaburi langu .jambo hilo
lilipelekee yule mama
kwenda kwa mganga wa
kienyeji na
kumbuka kuwa hakuna
mganga wa kienyeji
asiyetumia mizimu.
a kajikuta anahusika na mabo
mabaya zaidi hadi kumua mtoto
wake maana yule mzimu alianza
kwa kutaka damu ya kuku baadae
anataka kafara ya damu ya mtoto
wa yule mama maana ilifika
kipindi vitisho vikawa vyingi na
kwa sababu mama yule
alishaingia maagano na mizimu
ile kwa kutii maelekezo ya
kwanza akaanza kupata shinda
sana na akaambiwa atapata
mikosi maisha yake yote na hali
hiyo ikapelekee kuua mtoto wake
na cha ajabu shetani alimtumia
yule mganga wa kienyeji
kuongeza vitisho kwa mama na
kutoa ushauri wa kumwua mtoto.
Ndugu zangu jina la YESU
KRISTO pekee linaloweza
kuondoa mizimu maishani
mwako hivyo kama
unasumbuliwa na mikosi ya
ukoo, mizimu ya ukoo, utasa au
magonjwa ya ukoo basi kimbilia
kwenye maombezi katika kanisa
la kiroho karibu na wewe na
utafunguliwa na kuwa salama
kabisa mbali na laana zote za
ukoo na mashariti ya kishetani.
na katika BIBLIA kitambu cha
Mambo ya walawi 19:4 inasema
''Msigeuke kuandama sanamu, wala
msijifanyizie miungu ya kusubu
mimi ndimi BWANA, MUNGU
wenu .'' ndugu moja ya miungu
ambayo wanadamu wanaiabudu
ni mizimu na kumbuka kwamba
waganga wa kienyeji wanatumia
mizimu katika kazi zao na ndio
maana mama mmoja ambaye
sasa ameokoka alikua mganga
wa kienyeji zamani aliwahi
kuniambia kuwa kama mgojwa
mwenye majini akija kwake
kutibiwa yeye anachofanya
anaongeza majini ndani ya
mgojwa na kumpa mashariti ya
kufanya ili abaki mzima na moja
ya mashariti hayo alikua
anawaambia wateja kurudi kwake
kila baada ya miezi mitatu maana
anajua muda wa majini kutaka
ndamu umefika na kila mteja
akija lazima aje na kuku mwenye
rangi moja kama ni mweupe awe
mweupe pote na kama ni mweusi
awe mweusi pote.Katika 1
Samweli 28:7 BIBLAI inasema
''Ndipo Sauli akawaambia
watumishi wake, Nitafutieni
mwanamke mwenye pepo wa
utambuzi, nipate kumwendea na
kuuliza kwake. Watumishi wake
wakamwambia, Tazama, yuko
mwanamke mwenye pepo wa
utambuzi huko Endori.'' Huyu Sauli
alikua ni mfalme wa taifa la
Israel ambaye aliamua kuwafuata
waganga wa kienyeji na kitendo
hicho kilikua ni machukizo
makuu kwa MUNGU na kupelekea
kunyang'anywa ufalme akapewa
Daudi na huyo sauli akafa vitani
na jambo lile wa kwenda kwa
waganga liliongeza balaa kwa
taifa badala ya kupunguza .
Ndugu please please usikubali
kwenda kwa waganga wa kienyeji
wala usoma nyota maana
watakupoteza na utakua mbali
sana na MUNGU wako
aliyekuumba na hakika kwa
kitendo hivyo utakua
unajichimbia shimo mwenyewe.
ni hrei kumpelekea BWANA YESU
shida zako na yeye ni mwaminifu
na wa haki atakuponya na utakua
huru daima maana amesema
katika Mathayo 11:28 kwamba
'' Njoni kwangu, ninyi nyote
msumbukao na wenye kulemewa na
mizigo, nami nitawapumzisha''
MUNGU akubariki sana wewe
usiye na mizimu maishani mwako
maana ulimpa BWANA YESU
maisha yako na ukatengwa mbali
na mizimu ya ukoo ambao ipo
katika kila mtu ambaye
hajasafishwa kwa damu ya YESU
maana mizimu hiyo ipo tangu
kizazi na kizazi na mambo mengi
yanawapata ukoo fulani fulani tu
kwa sababu ya mizimu, ukielewa
hivyo chukua hatua kwa kumpa
YESU maisha yako na utakua
huru pia utakua ufunguo katika
ukoo wetu kuwafukuza mizimu ya
mababu ambayo imeleta balaa
kubwa katika maisha. maana
wapo watu wao wanajifahamu ni
watu wasio na akili shuleni yaani
ukoo mzima hakuna anayeweza
kufauli kwenda sekondari na
hawajui tatizo ni nini lakini
kumbe tatizo ni mizimu ya ukoo.
MUNGU akubariki na somo
litaendelea kwa kuangalia
mambo 6 kuhusu mizimu.

prepared by
Mwl israel kessy
phone 0759-627065  

Jumapili, 29 Novemba 2015

HEAVEN AND EARTH

extracted from the book of "genesis" it's all about some bibles cotations.
sorted and planned by
     Mwl israel kessy
Glory to God
           1-2First this: God created the Heavens and Earth—all you see, all you don't see. Earth was a soup of nothingness, a bottomless emptiness, an inky blackness. God's Spirit brooded like a bird above the watery abyss.

3-5God spoke: "Light!"
And light appeared.
God saw that light was good
and separated light from dark.
God named the light Day,
he named the dark Night.
It was evening, it was morning—
Day One.
6-8God spoke: "Sky! In the middle of the waters;
separate water from water!"
God made sky.
He separated the water under sky
from the water above sky.
And there it was:
he named sky the Heavens;
It was evening, it was morning—
Day Two.
9-10God spoke: "Separate!
Water-beneath-Heaven, gather into one place;
Land, appear!"
And there it was.
God named the land Earth.
He named the pooled water Ocean.
God saw that it was good.
11-13God spoke: "Earth, green up! Grow all varieties
of seed-bearing plants,
Every sort of fruit-bearing tree."
And there it was.
Earth produced green seed-bearing plants,
all varieties,
And fruit-bearing trees of all sorts.
God saw that it was good.
It was evening, it was morning—
Day Three.
14-15God spoke: "Lights! Come out!
Shine in Heaven's sky!
Separate Day from Night.
Mark seasons and days and years,
Lights in Heaven's sky to give light to Earth."
And there it was.
16-19God made two big lights, the larger
to take charge of Day,
The smaller to be in charge of Night;
and he made the stars.
God placed them in the heavenly sky
to light up Earth
And oversee Day and Night,
to separate light and dark.
God saw that it was good.
It was evening, it was morning—
Day Four.
20-23God spoke: "Swarm, Ocean, with fish and all sea life!
Birds, fly through the sky over Earth!"
God created the huge whales,
all the swarm of life in the waters,
And every kind and species of flying birds.
God saw that it was good.
God blessed them: "Prosper! Reproduce! Fill Ocean!
Birds, reproduce on Earth!"
It was evening, it was morning—
Day Five.
24-25God spoke: "Earth, generate life! Every sort and kind:
cattle and reptiles and wild animals—all kinds."
And there it was:
wild animals of every kind,
Cattle of all kinds, every sort of reptile and bug.
God saw that it was good.
26-28God spoke: "Let us make human beings in our image, make them
reflecting our nature
So they can be responsible for the fish in the sea,
the birds in the air, the cattle,
And, yes, Earth itself,
and every animal that moves on the face of Earth."
God created human beings;
he created them godlike,
Reflecting God's nature.
He created them male and female.
God blessed them:
"Prosper! Reproduce! Fill Earth! Take charge!
Be responsible for fish in the sea and birds in the air,
for every living thing that moves on the face of Earth."
29-30Then God said, "I've given you
every sort of seed-bearing plant on Earth
And every kind of fruit-bearing tree,
given them to you for food.
To all animals and all birds,
everything that moves and breathes,
I give whatever grows out of the ground for food."
And there it was.
31God looked over everything he had made;
it was so good, so very good!
It was evening, it was morning—
Day Six.
         By mwl israel kessy
You may call for prayers and counselling through
              Phone    0759-627065
                              0717-353059

Alhamisi, 19 Novemba 2015

In Jesus Christ there is happiness

     Leo ninataka niwaeleze kidogo kuhusiana na mambo ya kawaida kabisa kwa mwanadamu yeyote yule.

     Ifahamike hivi,mwanadamu yeyote yule awe ameokoka au la,anahitaji kuwa na raha ili maisha yake yawe sawasawa.bila furaha hauwezi kuwa amani kabisa.furaha ndio mwanzo wa mafanikio kabisa.unaweza kuuliza Israel unamaanisha nini kwa hilo.sikia"hauwezi kuwa na huzuni na ukaweza kutekeleza malengo yako hata kidogo.kumbuka biblia inasema huzuni za kidunia huleta jeraha ndani ya moyo ambapo husababisha mtu muda wote kuwaza tu huku akipoteza muda mwingi bila kufanya yampasayo kufanya.pia hata akifanya huwa hawezi kufikia lengo atakalo.sasa leo tuone tatizo kubwa la watu kukosa raha husababishwa na nini?

     1.ugomvi.pindi unapokuwa umegombana na mtu huwa amani inapotea automatically. Haijalishi utajaribu kuirudisha kiasi gani lakini haitakuwepo amani kabisaa.hii ni kwasababu hata biblia yenyewe inasema tafuteni kuwa naamani na watu wote na huo utukufu ambao hakuna mtu atakayeupata....ukiona hapo utagundua kuwa moja wapo ya sababu za kuwa na utukufu wa Mungu ndugu zangu ni kuwa na amani na kila mtu.sasa utaona amani ni muhimu hapo,kama amani ni muhimu basi ujue ya kuwa hakuna utukufu wa Mungu pasipo amani.sasa turudi katika hali ya kawaida,amani haiji isipokuwa furaha imetawala roho ya mtu.kama hauna furaha ndani ya moyo wako basi ujue amani haipo na kama amani haipo ujue utukufu haupo.

   Swali kwako wewe usomaye ujumbe huu.je?unaweza kuishi bila utukufu wa Mungu na ukafanikiwa.
      Mungu atusaidie katika tafakari hii ya leo na tafakari ijayo.
    
      By mwl israel kessy
Phone no 0759-627065