Alhamisi, 19 Novemba 2015

In Jesus Christ there is happiness

     Leo ninataka niwaeleze kidogo kuhusiana na mambo ya kawaida kabisa kwa mwanadamu yeyote yule.

     Ifahamike hivi,mwanadamu yeyote yule awe ameokoka au la,anahitaji kuwa na raha ili maisha yake yawe sawasawa.bila furaha hauwezi kuwa amani kabisa.furaha ndio mwanzo wa mafanikio kabisa.unaweza kuuliza Israel unamaanisha nini kwa hilo.sikia"hauwezi kuwa na huzuni na ukaweza kutekeleza malengo yako hata kidogo.kumbuka biblia inasema huzuni za kidunia huleta jeraha ndani ya moyo ambapo husababisha mtu muda wote kuwaza tu huku akipoteza muda mwingi bila kufanya yampasayo kufanya.pia hata akifanya huwa hawezi kufikia lengo atakalo.sasa leo tuone tatizo kubwa la watu kukosa raha husababishwa na nini?

     1.ugomvi.pindi unapokuwa umegombana na mtu huwa amani inapotea automatically. Haijalishi utajaribu kuirudisha kiasi gani lakini haitakuwepo amani kabisaa.hii ni kwasababu hata biblia yenyewe inasema tafuteni kuwa naamani na watu wote na huo utukufu ambao hakuna mtu atakayeupata....ukiona hapo utagundua kuwa moja wapo ya sababu za kuwa na utukufu wa Mungu ndugu zangu ni kuwa na amani na kila mtu.sasa utaona amani ni muhimu hapo,kama amani ni muhimu basi ujue ya kuwa hakuna utukufu wa Mungu pasipo amani.sasa turudi katika hali ya kawaida,amani haiji isipokuwa furaha imetawala roho ya mtu.kama hauna furaha ndani ya moyo wako basi ujue amani haipo na kama amani haipo ujue utukufu haupo.

   Swali kwako wewe usomaye ujumbe huu.je?unaweza kuishi bila utukufu wa Mungu na ukafanikiwa.
      Mungu atusaidie katika tafakari hii ya leo na tafakari ijayo.
    
      By mwl israel kessy
Phone no 0759-627065

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni