- Atom
Luka 12:40 - Nanyi jiwekeni
tayari, kwa kuwa saa msiyodhani
ndipo ajapo Mwana wa Adamu.
Maisha ya ushindi
▼
By mwl israel kessy
KUFUNGULIWA KUTOKA ROHO
ZA MIZIMU
Mizimu (family spirit) ni mapepo
yaliyotokana na malaika walioasi
pamoja na shetani ambayo watu
waliyafanya kama ndugu kutoka
kizazi hadi kizazi.
Mizimu no roho za shetani
ambazo ni chukizo kwa MUNGU
Kumbukumbu 18:9-12
''Utakapokwisha kuingia katika nchi
akupayo BWANA, MUNGU wako
usijifunze kutenda kwa mfano wa
machukizo ya mataifa yale.
Asionekane kwako mtu ampitishaye
mwanawe au binti yake kati ya
moto, wala asionekane mtu
atazamaye bao, wala mtu
atazamaye nyakati mbaya, wala
mwenye kubashiri, wala msihiri,
wala mtu alogaye kwa kupiga
mafundo, wala mtu apandishaye
pepo, wala mchawi, wala mtu
awaombaye wafu. Kwa maana mtu
atendaye hayo ni chukizo kwa
BWANA; kisha ni kwa sababu ya
hayo BWANA, MUNGU wako,
anawafukuza mbele
yako.'' yanayozungumza hapo
tuliposoma ni kuwahusu
WAGANGA WA KIENYEJI,
WACHAWI, WANAJIMU,WASIHIRI
NA WANAOWAOMBA WAFU,
mambo ambayo yote ni
machukizo kwa MUNGU na wote
hawa wanatumia mizimu
kufanikisha mambo yao na kwa
wale wanaomba maiti(wafu)
hawa wanaomba mizimu hivyo
wanahusika moja kwa moja na
mizimu maana mtu aliyekufa
hawezi kamwe kukusikia na hata
kama anakutokea usiku tambua
tu kwamba ni mizimu ambayo ni
majini yanavaa sura ya ndugu
yako na kuja kwako na kumbuka
kuwa jini anaweza kuiga kila kitu
kuanzia sauti hadi sura na kwa
sababu shetani anataka umkosee
MUNGU wako kwa kumtii yeye,
atakuambia mambo mengi ya
kufanya,
Yupo mama mmoja alikua
anatokewa na mama yake na
kumwambia kwamba '' siku hizi
umenisahau kabisa hata
kaburi langu hufagii hivyo
kesho asubuhi sana
kafagie na unyunyuzie
damu ya kuku juu ya
kaburi langu .jambo hilo
lilipelekee yule mama
kwenda kwa mganga wa
kienyeji na
kumbuka kuwa hakuna
mganga wa kienyeji
asiyetumia mizimu.
a kajikuta anahusika na mabo
mabaya zaidi hadi kumua mtoto
wake maana yule mzimu alianza
kwa kutaka damu ya kuku baadae
anataka kafara ya damu ya mtoto
wa yule mama maana ilifika
kipindi vitisho vikawa vyingi na
kwa sababu mama yule
alishaingia maagano na mizimu
ile kwa kutii maelekezo ya
kwanza akaanza kupata shinda
sana na akaambiwa atapata
mikosi maisha yake yote na hali
hiyo ikapelekee kuua mtoto wake
na cha ajabu shetani alimtumia
yule mganga wa kienyeji
kuongeza vitisho kwa mama na
kutoa ushauri wa kumwua mtoto.
Ndugu zangu jina la YESU
KRISTO pekee linaloweza
kuondoa mizimu maishani
mwako hivyo kama
unasumbuliwa na mikosi ya
ukoo, mizimu ya ukoo, utasa au
magonjwa ya ukoo basi kimbilia
kwenye maombezi katika kanisa
la kiroho karibu na wewe na
utafunguliwa na kuwa salama
kabisa mbali na laana zote za
ukoo na mashariti ya kishetani.
na katika BIBLIA kitambu cha
Mambo ya walawi 19:4 inasema
''Msigeuke kuandama sanamu, wala
msijifanyizie miungu ya kusubu
mimi ndimi BWANA, MUNGU
wenu .'' ndugu moja ya miungu
ambayo wanadamu wanaiabudu
ni mizimu na kumbuka kwamba
waganga wa kienyeji wanatumia
mizimu katika kazi zao na ndio
maana mama mmoja ambaye
sasa ameokoka alikua mganga
wa kienyeji zamani aliwahi
kuniambia kuwa kama mgojwa
mwenye majini akija kwake
kutibiwa yeye anachofanya
anaongeza majini ndani ya
mgojwa na kumpa mashariti ya
kufanya ili abaki mzima na moja
ya mashariti hayo alikua
anawaambia wateja kurudi kwake
kila baada ya miezi mitatu maana
anajua muda wa majini kutaka
ndamu umefika na kila mteja
akija lazima aje na kuku mwenye
rangi moja kama ni mweupe awe
mweupe pote na kama ni mweusi
awe mweusi pote.Katika 1
Samweli 28:7 BIBLAI inasema
''Ndipo Sauli akawaambia
watumishi wake, Nitafutieni
mwanamke mwenye pepo wa
utambuzi, nipate kumwendea na
kuuliza kwake. Watumishi wake
wakamwambia, Tazama, yuko
mwanamke mwenye pepo wa
utambuzi huko Endori.'' Huyu Sauli
alikua ni mfalme wa taifa la
Israel ambaye aliamua kuwafuata
waganga wa kienyeji na kitendo
hicho kilikua ni machukizo
makuu kwa MUNGU na kupelekea
kunyang'anywa ufalme akapewa
Daudi na huyo sauli akafa vitani
na jambo lile wa kwenda kwa
waganga liliongeza balaa kwa
taifa badala ya kupunguza .
Ndugu please please usikubali
kwenda kwa waganga wa kienyeji
wala usoma nyota maana
watakupoteza na utakua mbali
sana na MUNGU wako
aliyekuumba na hakika kwa
kitendo hivyo utakua
unajichimbia shimo mwenyewe.
ni hrei kumpelekea BWANA YESU
shida zako na yeye ni mwaminifu
na wa haki atakuponya na utakua
huru daima maana amesema
katika Mathayo 11:28 kwamba
'' Njoni kwangu, ninyi nyote
msumbukao na wenye kulemewa na
mizigo, nami nitawapumzisha''
MUNGU akubariki sana wewe
usiye na mizimu maishani mwako
maana ulimpa BWANA YESU
maisha yako na ukatengwa mbali
na mizimu ya ukoo ambao ipo
katika kila mtu ambaye
hajasafishwa kwa damu ya YESU
maana mizimu hiyo ipo tangu
kizazi na kizazi na mambo mengi
yanawapata ukoo fulani fulani tu
kwa sababu ya mizimu, ukielewa
hivyo chukua hatua kwa kumpa
YESU maisha yako na utakua
huru pia utakua ufunguo katika
ukoo wetu kuwafukuza mizimu ya
mababu ambayo imeleta balaa
kubwa katika maisha. maana
wapo watu wao wanajifahamu ni
watu wasio na akili shuleni yaani
ukoo mzima hakuna anayeweza
kufauli kwenda sekondari na
hawajui tatizo ni nini lakini
kumbe tatizo ni mizimu ya ukoo.
MUNGU akubariki na somo
litaendelea kwa kuangalia
mambo 6 kuhusu mizimu.