Jumanne, 27 Septemba 2016

               JE?WOKOVU NI NINI?NAO WATUSAIDIA NINI?
      
   

Bwana Yesu Kristo asifiwe ndugu katika Kristo Yesu.
    Wapendwa    Imempendeza Mungu leo tuangalie kwa kifupi nini maana ya wokovu.Mungu atusaidie na ayafungue masikio yetu ya ndani ili tuelewe na neno hili.Roho ambaye ni mwalimu wa kweli na atusaidie
         Sasa tutaenda kwa mtiririko huu
1.WOKOVU NI NINI?

     kwa lugha nyepesi kabisa na ya kawaida,wokovu ni hali ya kutoka katika hatari au hali mbaya au mabaya kuingia ktk mema.hiyo ni lugha nyepesi kabisa ambayo mtu yeyote anaweza kuelewa,

  Wokovu kibiblia ni:HALI YAKUHAMISHWA TOKA UFALME WA GIZA NA KUPELEKWA KATIKA KATIKA UFALME WA MUNGU,KATIKA NURU NA KUWA NURU KWELI KWELI,NI KUACHA DHAMBI KUMKIRI NA KUMKUBALI YESU KRISTO HUKU UKIAMINI KUWA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO. "kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa ni BWANA na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu,utaokoka,kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata Haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu" (warumi 10:9&10)
     Hapo tunaona yakuwa wokovu ni jambo lakiimani,,pasipo imani mtu yeyote hawezi kuokoka na sio tu kuokoka Bali hata kumpendeza Mungu.biblia inasema "wala pasipo imani haifai kumpendeza Mungu" 
    Kwahiyo wokovu ni kuhamishwa(kiroho) kutoka ufalme wa giza(yaani chini ya milki ya ibilisi shetani)na kuletwa katika ufalme wa NURU(yaani wa Mungu katika furaha,Amani na kushinda daima),kufa na kufufuka katika Kristo(na hapo hatuwi tena sisi Bali Kristo ndani yetu nguvu ya msalaba)   ".........................maana kwa kule kufa kwake,aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake,amwishia Mungu,vivyo hivyo nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Munguvkatika Kristo Yesu.

   Baada ya kuona kidogo maana ya wokovu sasa basi na tuelekee kipengele cha pili kuangalia je wokovu tukiupata ukiwa ndani mwetu utatusaidia nini? Karibu tuende pamoja

     2.WOKOVU UNATUSAIDIA NINI?

Wapendwa wengi sana ukiwauliza leo wokovu unawasaidia nini wengine watakuambia unawasaidia kwenda mbinguni tu na wengine watakuambia ni njia yakujipatia kitu fulani has a Mali na vitu vifananavyo na hivyo,
   pamoja na kwamba wokovu hutusaidia mambo mengi sana ila wacha tuone mambo makuu ambayo tunayapata tukiwa na wokovu

               WOKOVU HUTUSAIDIA MAMBO MAKUBWA MAWILI (2 main things)

  • Ni tiketi (ticket) ya kwenda mbinguni (Yohana 14:6,Tito 3:7)
  • Hutusaidia kuishi maisha ya furaha na maisha ambayo Mungu ametupangia kuishi katika kusudi lake hapa duniani.(ebrania 4:16)

   1.NI TICKET YA KWENDA MBINGUNI
 Tokea mwanzo Mungu alimuumba mwanadamu ili awe karibu naye,ili azungumze naye wazi,ili amuone waziwazi, lakini kutokana na dhambi aliyoifanya Adam katika bustani ya Eden ilimfanya Mungu awe mbali na wanadamu,dhambi ile iliufanya ulimwengu wote uwe chini ya laana ya dhambi ambayo hadi leo inausumbua ulimwengu, ndugu zangu napenda mjue hili,hata kama mtu anatenda mema kwa namna gani hawezi kusema ataenda mbinguni,hii ni kwa sababu mbinguni hatuendi kwa haki ipatikanayo kwa matendo yakisheria,la! Bali kwa imani kisha haki tuipatayo kwa NEEMA  ya Kristo Yesu.hakuna namna ambavyo unaweza kuingia mbinguni kama unategemea kwa matendo yako ndugu ila ni kwa kukiraribia kitu cha neema tu nyakati zote,wala sisi tuliookoka tusijisifu kwa kuwa tumeokoka,Bali tuzidi kukisogelea hicho kiti cha Rehema na neema "KWA MAANA MMEOKOLEWA KWA NEEMA,KWA NJIA YA IMANI AMBAYO HIYO HAIKUTOKANA NA NAFSI ZENU ILA NI KIPAWA CHA MUNGU.WALA SI KWA MATENDO MTU YEYOTE ASIJE AKAJISIFU" (waefeso 2:8&9) HALLELUYA..ndugu hakuna fahari kama hii yakukombolewa,maanake sio tu kwamba tunashinda katika ulimwengu huu ila pia tunazo ahadi za kuingia katika ufalme wa Mungu katika kutawala pamoja na Kristo baada ya dhiki za hapa.
       Wakati mwingine tutaendelea na kipengele cha pili,  Ila kwa sasa chukua hatua hii muhimu kwa kufuatilia kwa makini maneno haya muhimu hapa chini.

  Ndugu zangu wokovu si kitu cha kudharau wala kusema nitasubiria kesho au wakati mwingine maana hatuijui sekunde moja ya maisha yetu yajayo itakuwaje,Fikiria leo upo kesho haupo,leo unaishi kesho mwili umeacha roho,utaelekea wapi?Biblia inasema zipo hatima mbili, jehanamu na Paradiso ya milele,hakuna sehemu nyingine,je? wewe utapenda kwenda Jehanamu? naamini jibu litakuwa hapana kabisa,Kama usingependa kwenda jehanamu INA maana ungependa kwenda MBINGUNI,hivyo ni vyema kutengeneza mambo yako sasa,
    KAMA UPO TAYARI KUOKOKA FUATISHA MANENO HAYA NA CHUKULIA KWA IMANI KUWA NIWEWE UNAYASEMA TOKA MOYONI NA YESU ACHUNGUZAYE MIOYO ATAKUOKOA

   SEMA:ee Mungu baba, ninakuja kwako,mimi mwenyewe dhambi,ninaungama mbele zako dhambi zangu zote nilizozifanya,nakuja mbele za kiti chako cha neema nakusihi unisamehe na kunipa rehema.naomba ufute jina langu katika kitabu cha hukumu na kuandika jina langu katika kitabu cha uzima, asante Yesu kwa kuniokoa na kunifia pale msalabani,nipe kukujua wewe,nitembee ndani yako sikuzote,dhambi isinishinde,shetani asinishe,nidumu ndani yako siku zote za maisha yangu. 

      Ameen.
Umefanya uamuzi wa busara sana hii leo.Mungu wa mbinguni akutunze siku zote za maisha yako.2Timothy 4:18 biblia inasema ivi "Bwana ataniokoa na kila neno baya na kunihifadhi hata nifike ufalme wa MBINGUNI. Mungu akuhifadhi ndugu hata ufike salama

  Neema na iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo katika hali ya kutokuharibika
   By
              Mwalimu Israel Kessy

      Phone number     0783_872656

      e_mail address    israelkessy@gmail.com

      Facebook              Israel Kessy (mwalimu Kessy)